• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wachina waelekezwa pa kuwekeza.

    (GMT+08:00) 2018-12-04 20:48:52
    Waziri wa Viwanda, Bashara na Uwekezaji, Joseph Kakunda, amewataka wawekezaji wakuu 30 kutoka China waliokuja kuangalia nafasi za kuwekeza, kufanya hivyo katika viwanda vya kuongeza thamani ya bidhaa zinazozalishwa ndani, ili ziuzwe nje zaidi badala ya nchi kuendelea kuziagiza. Waziri aliyasema haya jijini Dar Es Salaam, kwenye kongamano la wafanyibiashara 30 kutoka China waliokutana na wazawa kwa lengo la kuhamasisha uwekezaji na kukuza biashara. Waziri Kakunda ambaye alisema kuwa China ni taifa linaloongoza kwa mitaji duniani, aliwasihi wafanyibiashara wa Tanzania kushirikiana nao na kujifunza mengi kutoka kwa wawekezaji hawa.

    Aidha, waziri aliwahakikishia wawekezaji hao kuwa watapata mazingira mazuri ya kufanyia shughuli zao, huku usalama ukipewa kipao mbele. Baadhi ya bidhaa ambazo waziri Kakunda anataka zitengenezwe ni pamoja na samani za ndani, kuchakata asali, kutengeneza bidhaa zinazotumika nyumbani kama vile runinga na simu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako