• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya chakula ya taifa ya Zimbabwe imefunga viwanda kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2018-12-05 09:04:09

    Kampuni kubwa ya uzalishaji wa chakula ya Zimbabwe imetangaza kufunga viwanda vyake viwili kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni. Kufungwa huko kwa muda usiojulikana kunatarajiwa kuathiri upatikanaji wa mikate, ambayo katika siku za karibuni bei yake ilipanda kutoka dola 1 na senti kumi na kuwa dola 1 na nusu. Waokaji wa mikate wametaja kupanda huko kwa bei kunatokana na kupanda kwa bei ya malighafi.

    Katika barua yake iliyotolewa wiki hii kwa wateja wake, kampuni hiyo imesema inakabiliwa na changamoto za kuwalipa wanaowauzia ngano kutokana na ukosefu wa fedha za kigeni, na kama ikishindwa kufanya hivyo itakosa ngano ndani ya wiki nne.

    Zimbabwe imekuwa inakabiliwa na uhaba wa fedha za kigeni, na kufanya iwe na upungufu wa bidhaa muhimu zinazoagizwa kutoka nje kama vile mafuta na dawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako