• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatarajia kukamilisha mageuzi ya nishati endelevu kabla 2020

    (GMT+08:00) 2018-12-05 09:07:13

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake inawekeza kwenye miradi ya nishati ya joto la ardhini, jua, upepo na maji ili kutimiza lengo la kukamilisha mageuzi ya nishati endelevu katika miaka miwili ijayo.

    Rais Kenyatta amesema serikali yake imeongeza megawati 1,063 za umeme kwenye gridi za taifa tangu aingie madarakani mwaka 2013.

    Akiongea kwenye halfahafla ya kuweka jiwe la msingi kwa mradi mmoja wa kuzalisha umeme kwa joto la ardhini huko Naivasha, rais Kenyatta amesema Kenya imeongeza juhudi za kuongeza matumizi ya aina mbalimbali za nishati endelevu, na iko mbioni kufikia lengo lake la kukamilisha mageuzi ya nishati kabla ya mwaka 2020.

    Ameongeza kuwa katika miaka mitano iliyopita tangu alipoingia madarakani, idadi ya familia zinaounganishwa na huduma ya umeme kote nchini Kenya imeongezeka na kufikia milioni 6.9, kutoka milioni 2.2 ya awali. Rais huyo pia amesisitiza ahadi yake kuwa atahahikisha kila nyumba nchini humo itapata huduma ya umeme kabla hajaondoka madarakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako