• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: CAF yaanika watakaowania tuzo ya mchezaji bora 2018

  (GMT+08:00) 2018-12-05 09:19:42

  Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), limetangaza majina 34 ya wachezaji wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kiume mwaka 2018. Pia kuna majina ya wachezaji 15 wa kike, wachezaji 6 vijana na makocha 10. Tuzo hizo zitatolewa Januari 8, 2019 jijini Dakar, Senegal.

  Matazamio ya mashabiki wengi kuwa mchuano mkali utakuwa kati ya Mohamed Salah anayekipiga Liverpool lakini raia wa Misri, Pierre Emerick Aubameyang raia wa Gabon anayechezea klabu ya Arsenal na Sadio Manne raia wa Senegal anayekipiga katika klabu ya Livepool ya Uingereza.

  Tuzo ya timu bora ya wanaume, timu za taifa zinazowania tuzo hizo ni Guinea Bissau, Kenya, Madagascar, Mauritania, Uganda na Zimbabwe. Na kwa upande wa timu bora ya taifa ya wanawake, timu zinazowania tuzo hii ni Cameroon, Ghana, Mali, Nigeria na Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako