• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China akutana na mwenzake wa Ureno

  (GMT+08:00) 2018-12-05 14:04:33

  Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Ureno Bw. Marcelo Rebelo de Sousa, na kukubaliana kuendelea kusukuma mbele ushirikiano wa kirafiki kati ya nchi zao, na kufungua ukurasa mpya wa maendeleo ya uhusiano kati yao.

  Rais Xi amesema, tangu miaka 39 iliyopita zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia, China na Ureno zinaendelea kushauriana, kuheshimiana, kuaminiana na kunufaishana, na uhusiano huo unaendelea kuimarika. Amesema China inaishukuru Ureno kwa kuendelea kufuata sera ya kuwepo kwa China Moja, na inapenda kushirikiana zaidi na Ureno katika masuala yanayohusu maslahi makuu na mambo yanayofuatiliwa zaidi na kila upande.

  Pia amesema, nchi hizo mbili zinapaswa kuongeza kwa kikamilifu ushirikiano chini ya mfumo wa Ukanda Mmoja na Njia Moja ili kupanua biashara ya pande mbili na kuhimiza ongezeko la ushirikiano.

  Kwa upande wake, Bw. de Sousa amesema Ureno inatarajia kuongeza ushirikiano na China katika sekta za biashara, fedha na utamaduni na kukaribisha makampuni ya China kuongeza uwekezaji nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako