• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wafanyakazi 55 wa Kenya wanaofanya kazi katika kampuni za China wapata tuzo ya wafanyakazi bora

    (GMT+08:00) 2018-12-05 18:46:48

    Chama cha uchumi na biashara cha China nchini Kenya kimefanya hafla ya kutoa tuzo kwa wafanyakazi bora 55 wa Kenya wanaofanya kazi katika kampuni za China kutokana na uhodari wao, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 55 tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kidiplomasia.

    Kaimu balozi wa China nchini Kenya Bw. Li Xuhang amesema, katika miaka 55 ya uhusiano huo, pande hizo mbili zimekamilisha miradi mikubwa zaidi ya mia moja, na kuongeza kuwa China ni mwenzi mkubwa wa biashara, uwekezaji na ukandarasi nchini Kenya.

    Kwenye hafla hiyo, ofisa wa wizara ya kilimo, biashara na ushirikiano wa Kenya Bw. Joseph Mbeya amesema, katika mwongo uliopita, biashara kati ya China na Kenya imeongezeka, na Kenya inatarajia kushirikiana zaidi na China katika kutimiza kunufaishana kwa pamoja.

    Wafanyakazi hao 55 wamepata nafasi ya kutembelea miji ya Beijing na Shanghai mwezi Aprili mwakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako