• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • EAC: Wafanyabiashara walalamikia mabadiliko ya mara kwa mara ya ushuru

  (GMT+08:00) 2018-12-05 19:45:52

  Wafanyabiashara ndogondogo wanaofanya shughuli zao maeneo ya mipakani katika nchi za Afrika Mashariki, wamelalamikia kuumizwa na uamuzi wa baadhi ya nchi ndani ya jumuiya hiyo.

  Hali hiyo imesababisha wengi wao kushindwa kunufaika na kutumia vyema fursa zinazojitokeza ndani ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-CM), ambalo limefungua milango kwa usafirishaji huru wa bidhaa na huduma.

  Wafanyabiashara hao wanasema mabadiliko ya ushuru wa forodha na marufuku ya mara kwa mara miongoni mwa nchi wanachama ni kikwazo kikubwa kwao.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa mipakani kutoka Kenya, Florence Atieno anasema uamuzi unapofanywa na baadhi ya nchi wanachama katika vikao vya juu, taarifa zake haziwafikii kwa wakati mwafaka.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako