• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NDONDI: Anthony Joshua awapa Tyson na Wilder wanachokitaka

  (GMT+08:00) 2018-12-06 08:30:04
  Hatimaye mbabe wa masumbwi duniani, Anthony Joshua amekubali kumpa pambano moja Tyson Fury baada ya kushuhudia matokeo ya sare kati ya bondia huyo na Deontay Wilder, wikendi iliyopita.

  Uamuzi huo wa Joshua umekuja kufuatia kauli nyingi za mashambulizi dhidi yake kutoka kwa Fury, ambaye baada ya pambano lake alidai kuwa Joshua ni muoga akimfananisha na kifaranga.

  Kupitia akaunti yake ya Twitter, Joshua alianza kwa kumsifu Fury ambaye ni Muingereza mwenzake kwa jinsi alivyoweza kupita kwenye pambano hilo.

  Fury na Wilder wamekuwa wakitamba kuwa Anthony Joshua anawakwepa na kwamba anachagua watu wa kupigana nao. Wilder amekuwa akidai kuwa timu ya Joshua inapotezea mpango wa pambano kati yao kwakuwa wanaogopa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako