• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • RIADHA: Mkenya aibuka mwanariadha bora wa kiume mwaka 2018

  (GMT+08:00) 2018-12-06 08:30:50

  Mkimbiaji wa mbio ndefu toka Kenya Eliud Kipchoge ndiye mwanariadha bora wa masafa marefu zaidi mwaka huu 2018. Kipchoge ametawazwa wadhifa huo mkubwa katika tasnia ya michezo kwenye hafla iliyoandaliwa na shirikisho la riadha duniani IAAF iliyofanyika Monte Carlo Monaco.

  Septemba mwaka huu, Kipchoge aliandika rekodi mpya ya mbio za Berlin kwa kukimbia kilomita 42 kwa muda wa saa 2 dakika 1 na sekunde 39.

  Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameongoza mamia ya wakenya kutuma salamu za pongezi kwa mwanariadha huyo kwa kuipeperusha vyema bendera ya Kenya.

  Kwa ujumla, Kipchonge ameshinda mashindano 10 ya riadha kati ya 11 aliyoshiriki toka alipong'oa nanga kwa mara ya kwanza mwaka 2013.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako