• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanafunzi watatu wa Tanzania washinda tuzo za mashindano ya TEHAMA ya kampuni ya Huawei

  (GMT+08:00) 2018-12-06 08:49:59

  Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amewatunuku vyeti wanafunzi watatu wa chuo kikuu ambao ni washindi wa tuzo za mashindano ya TEHAMA ya kampuni ya Huawei kwa kanda ya Kusini mwa Afrika mwaka 2018/19.

  Kampuni ya Huawei imesema washindi hao watajiunga na wanafunzi kutoka nchi nyingine za Kusini mwa Afrika, na kushiriki kwenye mashindano mengine yanayotarajiwa kufanyika mwezi Februari mwakani nchini Afrika Kusini na baadaye China, endapo watajitokeza na ushindi kwenye raundi ya pili.

  Bw. Majaliwa amesema mashindano hayo yamefanyika wakati serikali ya Tanzania inahitaji wataalamu wa TEHAMA kuunga mkono maendeleo ya viwanda nchini humo, na kwamba TEHAMA imesaidia kurahisisha mawasiliano na kupunguza urasimu kwenye serikali ya Tanzania.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako