• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la juu la Bunge la Afrika Kusini lapitisha ripoti kuhusu mageuzi ya ardhi

  (GMT+08:00) 2018-12-06 09:09:41

  Baraza la juu la bunge la Afrika Kusini limepitisha ripoti kuhusu mageuzi ya ardhi, inayoruhusu kutwaa ardhi bila fidia. Ripoti hiyo imepitishwa baada ya majimbo nane kati ya tisa kuridhia ripoti iliyowasilishwa mwezi uliopita na kamati ya mapitio ya katiba.

  Kwenye upigaji kura huo baraza la juu la bunge, Chama tawala cha ANC na chama cha upinzani cha EFF walipiga kura kuridhia ripoti hiyo, lakini chama cha DA kilipinga ripoti hiyo.

  Kufuatia hatua hiyo muswada wa sheria kuhusu utwaaji wa ardhi bila fidia utaandaliwa, na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali siku 30 kabla ya kutangazwa, ili kutoa fursa kwa wananchi kutoa maoni yao. Bunge litatakiwa kuupigia kura muswada huo siku 30 baada ya kufikishwa bungeni, na baadaye kusubiri saini ya rais kabla ya kuwa sheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako