• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wahimiza umuhimu wa masoko ya mitaji katika kuhimiza uwekezaji

  (GMT+08:00) 2018-12-06 09:10:21

  Umoja wa Afrika umesisitiza kuwa masoko ya mitaji ni muhimu katika utendaji wa masoko ya fedha barani Afrika na kuhimiza uwekaji wa akiba wa ndani na nje, pamoja na uwekezaji. Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika jana imesema kwa sasa masoko ya fedha ya Afrika yanadhibitiwa na taasisi za ndani na wawekezaji binafsi.

  Kuanzia mwaka 1989 masoko ya hisa yaliyo hai barani Afrika yameongezeka, hata hivyo masoko hayo yamekuwa ni madogo na yanagawanyika, na huwa yanaandikisha idadi ndogo ya makampuni.

  Umoja wa Afrika pia umesisitiza umuhimu wa kukusanya raslimali za ndani kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Umoja huo umesema kutumia raslimali za ndani kunaweza kuhimiza maendeleo ya muda mrefu ya Afrika na kuwaletea utajiri watu wake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako