• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Madaktari wa China kutoa matibabu bila malipo nchini Sudan

    (GMT+08:00) 2018-12-06 09:43:40

    Timu ya madaktari 8 wa China itafanya pasuaji 250 bila ya malipo kwa wagonjwa wa mtoto wa jicho nchini Sudan.

    Mradi huo unaojulikana kama "Brightness Action 2018" ulianzishwa na wizara ya afya ya Sudan na ofisi ya konsela wa uchumi na biashara ya Ubalozi wa China nchini Sudan. Waziri wa afya wa Sudan Bw. Mamoun Homeida amesema, Sudan na China zina uhusiano mzuri, na wizara yake pia imenufaika sana na ushirikiano na hospitali ya China.

    Naye mwakilishi wa ofisi ya konsela ya uchumi na biashara ya Ubalozi wa China nchini Sudan Bw. Zhou Chunlin amesema, mradi huo ni sehemu ya ushirikiano kati ya China na Sudan, na tangu mwaka 1970, China imetuma madaktari 34 kufanya kazi nchini Sudan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako