• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazindua mkakati wa kupanua upatikanaji wa umeme kwa wote kabla ya 2022

    (GMT+08:00) 2018-12-07 08:50:06

    Kenya imezindua mkakati wa kupanua upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wote kabla ya mwaka 2022.

    Waziri wa nishati wa Kenya Bw. Charles Keter amesema mjini Nairobi kuwa mkakati huo wa taifa KNES unaoungwa mkono na Benki ya dunia utatoa mpango wa kuziunganishia familia milioni tano na huduma ya umeme, na kazi hiyo ya kupanua upatikanaji wa huduma ya umeme kwa wananchi wote inakadiriwa kugharimu dola za kimarekani bilioni 2.75.

    Mbali na mradi wa KNES, serikali ya Kenya pia imezindua Mwongozo wa uwekezaji kwenye sekta ya umeme, unaotoa fursa za uwekezaji kwenye sekta hiyo ya nishati katika miaka mitano ijayo, ambazo zinakadiriwa kuwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 14.8.

    Bw. Keter pia amesema mpaka sasa asilimia 75 ya wakenya wameunganishwa na huduma ya umeme, ikilinganishwa na asilimia 32 ya mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako