• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zambia kupanua kazi ya upandaji miti ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa

    (GMT+08:00) 2018-12-07 09:24:58

    Zambia inapanga kuongeza idadi ya mikoa iliyoko kwenye mpango wake wa kupanda miti, ikiwa ni sehemu ya juhudi zake katika kupambana na madhara ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Waziri wa ardhi na maliasili wa Zambia Bibi Jean Kapata amesema serikali inapanga kuongeza idadi ya mikoa iliyoko kwenye mpango wa kupanda miti kutoka minne ya sasa hadi saba, kati ya mikoa yake kumi. Serikali ya Zambia inapanga kuwatumia wanafunzi milioni nne wa shule za msingi na sekondari, na baadhi ya watu kwenye familia kushiriki kwenye kazi ya upandaji miti.

    Serikali imesema inapanga kuhamasisha usambazaji wa miche kwenye mashule na kaya, huku viongozi wa jadi wakihimizwa kuwahamasisha watu ili kuhimiza upandaji wa miti.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako