• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yazitaka nchi za Afrika Mashariki kuoanisha mifumo yao ya forodha kuongeza ukusanyaji wa mapato

    (GMT+08:00) 2018-12-07 09:25:44

    Kenya imezitaka nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kuoanisha mifumo yao ya forodha ili kuimarisha ukusanyaji wa mapato. Kamishna mkuu wa mamlaka ya mapato ya Kenya Bw. John Njiraini ameliambia kongamano la kikanda kuhusu kodi mjini Nairobi, kuwa na mfumo unaofanana wa forodha, kutarahisisha ubadilishanaji wa taarifa, kuoanisha michakato ya biashara na kuanzisha mpango wa mawakala wa forodha.

    Bw. Njiraini amesema kwa sasa nchi za Afrika Mashariki zina forodha kumi za mipakani ambazo zinaunganishwa kwa mfumo mmoja, ili kupunguza utatanishi, muda na gharama za kuvuka mipaka.

    Naibu mkurugenzi wa Shirika la forodha duniani Bibi Brenda Mundia, amesema wanahamasisha kuwa na mfumo mmoja wa forodha ili uchangie maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kuhimiza mafungamano kati ya maeneo ya mipakani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako