• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baseball: Kiwanja kipya cha taifa mchezo wa Baseball chafunguliwa jijini Dar

  (GMT+08:00) 2018-12-07 10:13:10
  Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa jana amezindua kiwanja kipya cha taifa cha mchezo wa baseball na kuzindua mashindano ya taifa ya mchezo huo katika shule ya sekondari ya Azania jijini Dar es salaam.

  Kiwanja hicho kimejengwa kwa ushirikiano baina ya serikali ya Tanzania na serikali ya Japan.

  Bwana Majaliwa amewataka vijana kujikita kujifunza mchezo huo na si kuangalia soka peke yake, naye balozi wa Japan nchini Tanzania Shinichi Goto amesema Japan itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwemo ya michezo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako