• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mashindano ya kombe la Mfalme: Barca yafanya mauaji

  (GMT+08:00) 2018-12-07 10:15:25

  Timu ya soka ya Barcelona ya Uhispania imeibuka na ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya timu ya Cultural Leonesa kwenye mchezo wa marudiano hatua ya 16 bora kombe la mfalme wa Hispania usiku wa jana mchezo uliochezwa uwanja wa Camp Nou.

  Mshambuliaji wa timu hiyo Denis Suarez amefunga mabao 2, huku Munir akifunga katika dakika ya 18 na Malcom dakika ya 43, goli la kufutia machozi la Cultural Leonesa limefungwa na Joseph Sene dakika ya 54.

  Barca inasonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-1 baada ya kushinda ugenini katika mchezo wa kwanza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako