• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa watoa ripoti mpya

    (GMT+08:00) 2018-12-07 18:21:57

    Sekretarieti ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia makubaliano ya utaratibu wa mabadiliko ya hali ya hewa imetoa ripoti mpya ikisisitza maendeleo na pengo la utekelezaji wa operesheni ya hali ya hewa ya nchi zilizoendelea kabla ya mwaka 2020.

    Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano wa mbadiliko ya hali ya hewa uliofanyika huko Katowice imesema, kuanzia mwaka 1990 hadi 2016, utoaji wa hewa chafu wa nchi zilizoendelea ulipungua kwa asilimia 13. Wakati huohuo, hatua zilizochukuliwa na nchi zilizoendelea za kupunguza utoaji wa hewa chafu zimeongezeka na kupata mafanikio. Kwa mujibu wa makubaliano ya Paris, hatua hizo ni msingi muhimu wa kuharakisha utekelezaji wa operesheni za hali ya hewa baada ya mwaka 2020.

    Ripoti hiyo pia imesema, nchi zilizoendelea zimeunga mkono utoaji wa mitaji kwa nchi zinazoendelea ili kuhimiza nchi hizo kuelekea njia ya kujiendeleza ya kupunguza utoaji wa hewa chafu na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako