• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yarusha chombo cha uchunguzi cha Changé-4 kujua mambo yaliyojificha ya upande wa pili wa mwezi

  (GMT+08:00) 2018-12-08 18:15:52

  Chombo cha uchunguzi wa mwezini cha Changé-4 kimerushwa leo mapema alfajiri katika kituo cha kurushia satelite cha Xichang mkoani Sichuan, na kinatarajiwa kutua bila matatizo kwa mara ya kwanza katika upande wa pili wa mwezi.

  Kwa mujibu wa Idara ya Taifa ya Anga ya juu ya China CNSA, kazi ya chombo cha Changé-4 ambayo ni hatua muhimu ya kufumbua mambo yasiyojulikana ya upande wa pili wa mwezi, itakuwa ni pamoja na uchunguzi wa kinajibu wa mawimbi madogo ya redio, kutafiti ardhi ya mwezi na maumbile yake, kugundua uundwaji wa madini na muundo wa uso wa ardhi, na kupima mionzi ya nutroni na atomi isiyo na sifa zilizo bayana ili kuchunguza mazingira ya upande wa pili wa mwezi.

  Majaribio ya kisayansi na kiteknolojia yaliyobuniwa na vyuo vikuu vya China, yatafanywa mwezini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako