• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • CERF yachangiwa dola za kimarekani milioni 439

    (GMT+08:00) 2018-12-08 18:18:09

    Kwenye mkutano wa ngazi ya juu wa mfuko wa kukabiliana na hali ya dharura wa Umoja wa Mataifa, wafadhili wamechangia dola za kimarekani milioni 439 kwa mwaka 2019, kiasi ambacho kimefikia rekodi ya juu kwa mfuko huo.

    Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe zaidi ya 150 kutoka nchi 60 wanachama wa Umoja wa Mataifa, na nchi 41 kati yao zimetangaza kuchangia kwa ajili ya mwaka 2019.

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, kila mwaka mfuko huo umetoa msaada na hifadhi kwa maisha ya mamilioni ya watu, kuhakikisha msaada wa kibinadamu unawafikia watu wanaokabiliwa na msukosuko kwa haraka na kwa njia yenye ufanisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako