• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Canada inalinda haki za binadamu za nani?

    (GMT+08:00) 2018-12-09 17:58:07

    Ofisa mkuu wa fedha wa kampuni ya Huawei wa China Bibi Meng Wanzhou alikamatwa nchini Canada tarehe 1 Desemba, kutokana na ombi la Marekani. Kesi yake ilisikilizwa Ijumaa mjini Vancouver, lakini uamuzi bado haujatolewa na itaendelea kusikilizwa kesho.

    Kukamatwa kwa bibi Meng kunafuatiliwa na jumuiya ya kimataifa, na kuonyesha ukweli mbele ya dunia kuhusu kukamatwa kwake.

    Kwanza, Marekani na Canada zinajidai kuwa na mfumo kamili wa sheria, haki na usawa. Lakini tukio hilo linaonyesha kuwa haki za utekelezaji wa sheria zimekuwa maneno matupu, na kuonyesha kiini chake cha umwamba na ukorofi.

    Pili, kitendo cha Canada kupuuza haki za binadamu kimeonyesha inatumia vigezo tofauti katika mambo ya haki za binadamu, inaharibu vitendo vya ulinzi wa haki za binadamu, na maendeleo ya amani na utulivu wa dunia.

    Tatu, tukio hilo ni mapambano dhidi ya makampuni ya sayansi na teknolojia ya China, ni dhahiri kuwa Canada inafanya kazi ya kuleta madhara.

    Nne, kitendo hiki cha Canada cha kumkamata bibi Meng kinafuatiliwa sana na jamii ya China, sura ya Canada kwa wachina imeshuka chini. na kitendo hiki kitaathiri vibaya uhusiano kati ya China na Canada.

    "Kumwachia huru mara moja bibi Meng Wanzhou" ni ombi halali la kampuni ya Huawei na serikali ya China. China inatumai serikali ya Canada na idara za utekelezaji wa sheria kutoenda kinyume cha haki na usawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako