• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rekodi ya Man City ya kutofungwa ligi kuu Uingereza yakatishwa na Chelsea

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:30:54

    Pamoja na kuonekana kuwa ni timu ngumu isiyoweza kufungika kwa sasa kwenye ligi kuu nchini Uingereza kutokana na Ubora wake, klabu ya Manchester City usiku wa kuamkia jumapili hii imeshindwa kuandika rekodi ya kupata ushindi mara 8 baada kufungwa kwa magoli 2-0 na timu ya Chelsea ambayo inafanya vizuri pia katika msimu huu.

    Chelsea ilipata magoli yake kupitia Ngolo Kante kunako dakika ya 45, na David Luiz katika dakika ya 78, na timu hiyo sasa imepanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo baada ya kufikisha alama 34 sawa na timu ya Arsenal inayoshika nafasi ya tano.

    Na kufuatia matokeo hayo, Manchester City ambayo imefungwa kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye ligi kuu inashuka hadi nafasi ya pili kwa kubaki na alama 41 ilizo nazo, na nafasi ya kwanza ikichukuliwa na Liverpool yenye alama 42 baada ya ushindi iliopata jumamosi dhidi ya AFC Bournemouth, na Liverpool ndiyo timu pekee ambayo haijafungwa mpaka sasa kwenye ligi hiyo baada ya kucheza mechi 16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako