• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makubaliano ya Brexit ya Bibi May yashindwa kutoa ufafanuzi wazi

    (GMT+08:00) 2018-12-10 08:40:58

    Kamati ya Baraza la makabwela la bunge la Uingereza kuhusu makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya, imekubaliana kwa kauli moja kuwa makubaliano ya Brexit ya waziri mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May, yameshindwa kuweka wazi mustakbali wa nchi.

    Ripoti hiyo yenye ukosoaji mkali imetolewa saa 48 kabla ya upigaji kura ndani ya bunge kuhusu kuidhinisha au kukataa makubaliano hayo. Kamati imesema kwenye ripoti yake kuwa baada ya miezi 20 tangu majadiliano ya Brexit yaanze, kinachofahamika wazi ni makubaliano ya Uingereza kujitoa, lakini hakuna maelezo ya kutosha kuhusu uhusiano wa baadaye kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

    Ripoti pia inasema makubaliano hayo hayajaweka wazi uhusiano wa kibiashara kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya utakuwa vipi, baada ya kipindi cha mpito kinachotarajiwa kumalizika mwezi Desemba mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako