• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Ligi kuu Tanzania Bara, Yanga yaitoea nyuma na kuifumua Biashara United

  (GMT+08:00) 2018-12-10 08:51:59

  Yanga SC imerejea kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania bara baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Biashara United ya Musoma mchezo uliopigwa uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.

  Ushindi huo unaifanya Yanga ifikishe alama 41 baada ya kucheza mechi 15 na kukalia usukani wa ligi hiyo, Azam FC yenye alama39 ambao wanarejea nafasi ya pili wakati mabingwa watetezi Simba SC wanaendelea kukamata nafasi ya tatu.

  Biashara United ndio walikuwa wa kwanza kufungua mlango wa mabao walipopata bao katika dakika ya 38 lililofungwa na Abdulmajjid Mangalo, baada ya bao hilo liliwashtua Yanga na kocha wao Mwinyi Zahera kufanya mbadiliko yaliyozaa matunda na yanga kusawazisha bao kupitia kwa Abdallah Hajji Shaibu dakika ya 70, Yanga ilipata goli lake la pili lililowekwa kimiani na mkongo Heritier Makambo dakika ya 80 na kufanya hadi refa anapuliza kipyenga kumaliza mechezo huo, Yanga waliondoka na ushindi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako