• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nigeria yatarajia ongezeko la uchumi kutokana na uwekezaji wa dola milioni 600 kwenye madini chuma

    (GMT+08:00) 2018-12-10 09:32:07

    Serikali ya Nigeria inatarajia uwekezaji wa dola milioni 600 za kimarekani kwenye kuzalisha na kuchakata chuma utahimiza ukuaji wa uchumi nchini humo.

    Waziri wa fedha wa nchi hiyo Bibi Zainab Ahmed amethibitisha kuwa Nigeria imesaini makubaliano na Kampuni ya maliasili na madini ya Afrika, ambayo ni mwekezaji wa kigeni katika sekta ya migodi na chuma.

    Waziri huyo amesema makubaliano hayo yanalenga kuimarisha sekta ya madini nchini humo, na huu ni uwekezaji mkubwa zaidi kupatikana katika sekta ya madini ya Nigeria katika miongo miwili iliyopita, ambao utatoa ajira 3,500 za moja kwa moja, na nyingine maelfu zisizo za moja kwa moja.

    Pia amesema mradi huo unatarajiwa kuhimiza maendeleo ya viwanda na jamii, na kuongeza uzalishaji wa umeme na bidhaa nyingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako