• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yapiga hatua kubwa katika kulinda haki za binadamu

  (GMT+08:00) 2018-12-10 17:20:36

  Leo tarehe 10 ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Mkutano wa kuadhimisha miaka 70 tangu Umoja wa Mataifa utoe "Azimio la Haki za Binadamu Duniani" umefanyika mjini Beijing. Katika miaka 70 iliyopita, China imepata mafanikio makubwa yanayojulikana duniani katika kuheshimu na kulinda haki za binadamu.

  "Azimio la Haki za Binadamu Duniani" lililopitishwa na Baraza kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba mwaka 1948, ni azimio lenye maana kubwa katika historia ya ustaarabu wa binadamu, na kuleta athari kubwa kwa maendeleo ya shughuli za haki za binadamu duniani. Mkuu wa idara ya uenezi ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Wang Kunming anasema,

  "Tunahakikisha haki za kuishi na kujiendeleza za wananchi wote. Mazingira ya kuishi na kujiendeleza ya watu nchini China yameboreshwa kwa kiasi kikubwa, na wastani wa kuishi kwa watu uliongezeka na kuwa miaka 76.7 ya mwaka jana kutoka chini ya 35 ya mwaka 1949. Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, idadi ya watu maskini imepunguzwa kwa milioni 740."

  Licha ya hayo, China pia imejenga mfumo maalumu wa sheria ili kuhakikisha haki za binadamu. Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa haki za binadamu cha Chuo Kikuu cha Nankai, ambaye pia ni mtendaji wa taasisi ya utafiti wa haki za binadamu ya China Bw. Chang Jian amesema, China imechagua njia pekee ya kuendeleza haki za binadamu kwa kuunganisha kanuni ya "Azimio la Haki za Binadamu Duniani" na hali halisi ya China. Anasema, )

  "China inaona haki za kuishi na kujiendeleza ni haki kuu za binadamu, na imehimiza maendeleo ya haki nyingine za binadamu kwa kuhakikisha haki hizo kuu. China pia inaona haki mbalimbali za binadamu zinategemeana, na kuhimiza uwiano wa maendeleo ya haki za uchumi, jamii, utamaduni, na mazingira, na haki za siasa. Aidha, China pia inazingatia kulinda haki za watu maalumu, haswa watu wa makabila madogo, wanawake, watoto na walemavu. China inatetea kufikia maelewano na maoni ya pamoja kuhusu haki za binadamu kupitia mazungumzo."

  Ingawa shughuli za haki za binadamu zimepiga hatua kubwa, lakini bado zinakabiliwa na changamoto kubwa. Hivi sasa zaidi ya watu milioni 700 wanakumbwa na umaskini, na miongoni mwao zaidi ya milioni 132 wanahitaji msaada wa haraka wa kibinadamu. Mkurugenzi wa idara ya mambo ya kimataifa ya wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Li Xuejun amesema, nchi mbalimbali zinapaswa kushirikiana vizuri ili kusukuma mbele shughuli za haki za binadamu duniani. Anasema,

  "Kwanza ni kuanzisha mazingira ya amani na utulivu duniani, pili ni kulinda haki na usawa duniani, tatu ni kuhimiza na kulinda haki za binadamu kupitia maendeleo, na nne ni kuzingatia zaidi watu wakati wa kuendeleza uchumi."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako