• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Mauritius yaongoza kwa uwekezaji Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-12-10 18:40:17

    Benki kuu ya Rwanda imesema kuwa wawekezaji wa Mauritius ndio wamewekeza kiwango kikubwa cha fedha nchini humo.

    Benki hiyo imesema wawekezaji hao wamejikita kwenye sekta za utalii, kawi na utengenezaji bidhaa.

    Kulingana na takwimu za benki hiyo uwekezaji wa Mauritius ulifikia asilimia 25.8 mwaka 2017 ambao ni dola milioni 117.

    Aidha benki hiyo inasema mwaka 2017 mtaji wa kigeni nchini Rwanda ulikuwa dola milioni 452 ikilinganishwa na dola milioni 542 za mwaka 2016.

    China ndio mwekezaji wa pili nchini Rwanda ikiwa imewekeza dola milioni 81 hasa kwenye sekta ya utengenezaji bidhaa, na kufuatiwa na india inayowekeza dola milioni 31 hasa katika Tehama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako