• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe: Sekta ya dawa Zimbabwe yakabilia na upungufu wa fedha za kigeni

    (GMT+08:00) 2018-12-10 18:40:48

    Sekta ya dawa nchini Zimbabwe imesema imekuwa vigumu kuagiza madawa kutokana na upungufu wa fedha za kigeni.

    Rais wa chama cha wauza madawa nchini humo Portifa Mwendera aliiambia Kamati ya Afya kuwa sekta hiyo inadaiwa na wauzaji wa dawa wa kigeni dola milioni 38M, kutoka $ 13M mwezi Oktoba mwaka jana.

    Alisema kutokana na kukosa uwezo wa kulipa, wauzaji wa nje sasa wanahitaji kulipwa kwanza hali ambayo imewalazimu kulipisha bidhaa zao kwa dola za kimarekani.

    Mwendera amesema sasa wanakabiliwa na uhaba wa madawa ya kupunguza maumivu, na kisukari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako