• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Wakenya zaidi kuunganishwa na umeme

  (GMT+08:00) 2018-12-10 18:41:52

  Serikali ya Kenya imeanza kujadili mpango wa shilingi bilioni 270 wa kunganisha nyumba zote na umeme nchini humi.

  Wizara ya kawi imesema inapanga kuunganisha nyumba milioni 5 na umeme ndani ya miaka 4 ijayo.

  Waziri wa kawi Charles Keter amesema mpango huo utatekelezwa kwa ushirikiano na serikali ya Kenya pamoja na washirika kama vile benki ya dunia na benki ya maendeleo ya Afrika.

  Chini ya mpango huo wakenya watahitajika kulipa shilingi 15,000 pole pole ili kunganishwa na umeme.

  Waziri Keter amesema sekta ya kibinafsi itawekeza fedha zingine shilingi bilioni 45 za kuunganisha nyumba milioni 2 kwa kawi ya jua.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako