• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mahakama ya Ulaya yasema Uingereza iko huru kufuta kipengele cha 50 na kuzuia Brexit

  (GMT+08:00) 2018-12-10 18:58:42

  Mahakama ya Ulaya imesema, Uingereza iko huru kufuta kwa pande zote taarifa yake ya kudhamiria kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya (EU).

  Uamuzi uliochapishwa kwenye tovuti ya mahakama hiyo umesema, hatua hiyo, ikiamuliwa kuendana na mahitaji ya katiba ya nchi hiyo, itakuwa na maana kuwa Uingereza itaendelea kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya chini ya kanuni ambazo hazijabadilishwa kutokana na hadhi yake kama nchi mwanachama.

  Uamuzi huo, uliofikiwa na kundi la wanasiasa wa Kiskoti, utatoa msukumo kwa watu wanaotaka kura ya maoni ifanyike kwa mara ya pili nchini Uingereza, ambao pia wanataka kuzuia nchi hiyo kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako