• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM waunga mkono mpango wa Kenya wa kupanua upatikanaji wa huduma za afya kwa kila mwananchi

    (GMT+08:00) 2018-12-11 08:59:00

    Shirika la afya duniani WHO limeunga mkono mpango wa Kenya wa kupanua upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wote UHC, ambao ni sehemu ya ajenda ya Big Four ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.

    Katibu mkuu wa WHO Bw. Tedros Adhanom Ghebreyesos amesema atawahamasisha viongozi wa shirika hilo kuhudhuria hafla ya uzinduzi wa mpango huo, ambao utatekelezwa kwanza katika kaunti nne kati ya 47 nchini Kenya. Pia amemhakikishia rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kuwa WHO itaunga mkono kithabiti mpango huo, na kuitaja Kenya kuwa ni mtangulizi barani Afrika.

    Wizara ya afya ya Kenya imesema kaunti za Kisumu, Isiolo, Nyeri na Machakos zitakazotekeleza mpango huo kwanza, zitakuwa kielelezo cha utekelezaji wa mpango huo katika nchi nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako