• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu wa Uingereza amethibitisha kuahirishwa upigaji kura kuhusu Brexit

    (GMT+08:00) 2018-12-11 09:26:52

    Waziri Mkuu wa Uingereza Bibi Theresa May amethibitisha kuwa upigaji kura kwenye bunge la Uingereza kuhusu makubaliano ya kujitoa Umoja wa Ulaya, umeahirishwa.

    Bibi May amesema suala la mpaka kati ya Ireland Kaskazini na Umoja wa Ulaya lina upinzani kutoka kwa wabunge, na serikali ingeshindwa vibaya kwenye upigaji kura huo.

    Uamuzi huo ulifikiwa saa chache baada ya ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza kutangaza kuwa upigaji kura huo utafanyika kama ilivyopangwa. Bibi May amesema atafanya mazungumzo ya dharura na Umoja wa Ulaya kuhusu suala la mpaka ya Ireland Kaskazini.

    Wakati serikali ya Uingereza ikitafakari cha kufanya kuhusu hali hiyo, Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amedokeza kuwa Marekani inaweza kufikiria kusaini makubaliano ya biashara huria na Uingereza, hata kama ikijitoa Umoja wa Ulaya bila makubaliano yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako