• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Nigeria asema Afrika inakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na ufisadi

    (GMT+08:00) 2018-12-11 10:00:12

    Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria amesema Bara la Afrika linakabiliwa na athari mbaya zinazotokana na ufisadi tangu lipate uhuru, akisema ni muhimu kuchukua hatua ili kubadilisha hali hiyo.

    Rais Buhari amewaagiza viongozi wa Nigeria kuendelea kutekeleza sera zitakazojenga mfumo wa kupambana na maofisa mafisadi.

    Akiongea kwenye mkutano wa Mafunzo ya ufanyaji tathmini ya hatari ya ufisadi kwa wakuu na maofisa waandamizi wa mashirika ya kupambana na ufisadi ya Umoja wa Afrika, Rais Buhari amesema Nigeria imechukua hatua za kujenga uaminifu na uwazi kwenye serikali, na kuwawajibisha wanaoshitakiwa kuiba rasilimali za taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako