• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC yaanzisha msako mkali dhidi ya matapeli wa ubadilishaji pesa za kigeni. .

    (GMT+08:00) 2018-12-11 19:05:55

    Serikali za jumuiya ya Afrika Mashariki, zimeshirikiana kuanza vita vikali dhidi ya biashara haramu ya ubadilishaji wa pesa. Hatua ya hivi punde ni benki kuu za mataifa ya Afrika Mashariki kuweka masharti makali kwa wamiliki wa biashara hii ya ubadilishaji pesa. Wabadilishaji wa pesa haramu wamesababisha mfumko na kupunguza thamani ya sarafu za Afrika Mashariki. Hii huathiri uagizaji wa bidhaa kutoka mataifa mengine kwa sababu bei yake hupanda zaidi. Nchini Tanzania, shilingi ilipungua thamani kwa asilimia 0.3 kati ya Septemba na Oktoba mwaka huu. Kulinga na ripoti ya StratLink , thamani ya shilingi imekuwa ikipungua kwa wastani wa asilimia 2.2 kwa miezi kumi iliyopita. Maafisa wa usalama na mashirika mengine ya serikali kutoka Rwanda, Uganda, Kenya na Tanzania yamekaza kamba na kuwatia mbaroni wabadilishaji haramu wa pesa za kigeni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako