• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda yazindua mpango wa kutafiti maendeleo ya mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:02:01

    Wizara ya afya ya Uganda imezindua mpango wa tatu wa kuangalia maendeleo yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya Uganda imesema kutakuwa na upimaji wa miezi miwili wa sampuli ya nchi nzima, wenye lengo la kupata takwimu kuhusu uwepo wa ugonjwa wa malaria, mazingira ya hatari za ugonjwa huo, ujuzi wa watu kuhusu ugonjwa huo. Upimaji huo utahusisha wanawake wenye umri kati ya miaka 15 na 49, kwenye takriban kaya elfu 9 katika nchi nzima.

    Ugonjwa wa Malaria ni ugonjwa unaosababisha vifo vya watu wengi nchini Uganda, hasa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na kina mama wajawazito.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako