• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Neymar kasaini dili litakalomzuia kwenda Real Madrid na Barcelona

  (GMT+08:00) 2018-12-12 09:05:25

  Tukiwa tunaelekea kufunguliwa kwa dirisha la usajili la mwezi Januari Neymar alikuwa ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kutawala vichwa vya habari juu ya kuihama Paris Saint Germain na kujiunga na Real Madrid ya Hispania, hiyo ni baada ya kuhusishwa na Real Madrid toka dirisha la usajili la majira ya joto. Kusaini kwa Neymar kwa mkataba wa matangazo ya kibiashara na National Bank Of Qatar kunaondoa nafasi ya Neymar kuihama PSG hivi karibuni, Neymar yupo PSG timu ambayo inamilikiwa na familia ya kifalme ya Qatar, hivyo mkataba wake na QNB unatajwa kutomuwezesha kwenda nje ya PSG. Mkataba huo ambao baadhi ya vipengele vimewekwa kama siri, vinatajwa kuipa haki Bank hiyo ya kusimamia hakimiliki ya picha za Neymar, hata hivyo uwezekano unakuwa mdogo kwa Neymar kuondoka PSG kutokana na QNB kutaka staa huyo abakie PSG kwani wanaidhamini timu hivyo ni rahisi kwao kunufaika na ubalozi wa Neymar akiwa anaichezea timu wanayoidhamini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako