• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la UN laifurahia UNAMID katika mchakato wa ujenzi mpya wa amani Darfur

    (GMT+08:00) 2018-12-12 09:45:23

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha maendeleo ya tume ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika eneo la Darfur UNAMID kutokana na mchakato wake wa kuiboresha, pia limesisitiza tena kuunga mkono ujenzi mpya wa amani na maendeleo ya Darfur.

    Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema inafurahia hali ya usalama ya Darfur iliyoko nje ya eneo la Jebel Marra imeboreshwa, na kusisitiza kuendelea kuzikabidhi baadhi ya maeneo yaliyosimamiwa na UNAMID kwa serikali ya Sudan.

    Baraza hilo limesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa vigezo vya mafanikio kwenye mkakati wa kuondoka kwa tume ya UNAMID, kwenye ripoti kuhusu Sudan na Sudan Kusini aliyoitoa tarehe 12 Oktoba. Baraza limetaka katibu mkuu na mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika watoe ripoti za siku 90 juu ya maendeleo ya kazi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako