• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mradi wa kupeleka maji kutoka sehemu ya kusini hadi sehemu ya kaskazini wanufaisha watu milioni 100

  (GMT+08:00) 2018-12-12 17:12:32

  Tarehe 12 Disemba mwaka 2014, kipindi cha kwanza cha mstari wa kati wa mradi wa kupeleka maji kutoka kusini hadi kaskazini nchini China kilikamilika, na maji kutoka Mto Changjiang yalianza kupatikana katika sehemu ya kaskazini. Katika miaka minne iliyopita, maji yaliyohamishwa kupitia mstari wa kati na mstari wa mashariki wa mradi huo yalifikia tani bilioni 22.2. Mistari hiyo miwili imekuwa chanzo kikuu cha upatikanaji maji kwa zaidi ya miji 40 ya kaskazini, na kunufaisha zaidi ya watu milioni 100.

  Mradi wa kusafirisha maji kutoka kusini hadi kaskazini nchini China ni mradi mkubwa zaidi wa kusafirisha maji duniani. Mstari wa mashariki na wa kati iliyoko, imeongeza uwezo wa utoaji wa maji wa miji iliyoko kando ya mistari hiyo kwa kiasi kikubwa, na imekuwa chanzo kikuu cha upatikanaji wa maji kwa zaidi ya miji 40 mikubwa na ya kati ikiwemo Beijing na Tianjin. Naibu mkurugenzi wa idara ya maji ya China inayoshughulikia mradi wa kusafirisha maji kutoka kusini hadi kaskazini Bw. Yuan Qitian anasema,

  "Uwezo wa kutoa maji wa miji hiyo umeongezeka kwa kiasi kikubwa, na maji yanayosafirishwa kutoka kusini yamewanufaisha watu zaidi ya milioni 100 wa sehemu ya kaskazini."

  Aidha, mradi wa kusafirisha maji kutoka kusini hadi kaskazini pia umekuwa na manufaa kwa mazingira. Mwezi Septemba mwaka huu, China ilijaribu kuweka maji ya kusini kwenye mito mitatu ya sehemu ya kaskazini. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya uongozi wa juhudizya kupambana na maafa ya maji ya mkoa wa Hebei Bw. Yu Qingtao anasema,

  "Tuliweka maji kwa mito mitatu ya Juma, Hutuo na Fuyang. Madhumuni yetu ni kwamba, maji hayo yataingia ardhini ili kuongeza kiwango cha maji chini ya ardhi. Tuliweka vituo 70 vya uchunguzi, na kupata takwimu zinazoonesha kuwa wastani ya kiwango cha maji chini ya ardhi umeongezeka kwa nusu mita."

  Hatua hii pia ilifufua mto Hutuo ambao ulikuwa umekauka kwa miongo kadhaa. Sasa mto huo umekuwa sehemu ya kuvutia. Bw. Shi Xiaoxu anaishi karibu na mto huo. Anasema,

  "Nilisoma katika shule ya sekondari iliyoko kando ya Mto Hutuo. Zamani mto huo ulikuwa na mchanga tu, na kuleta vumbi kwa wingi. Mkoa wa Hebei una upungufu wa maji, haswa mji wa Shijiazhuang. Baada ya kuwekwa maji, mto huo unawavutia watu wengi. Wakati wa wikiendi, nakuja hapa kucheza na mtoto wangu."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako