• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Benki Kuu ya Kenya yatoa sarafu mpya

    (GMT+08:00) 2018-12-12 18:30:02

    Benki Kuu ya Kenya imetoa sarafu mpya zenye na michoro ya wanyama.

    Sarafu hizo nne ni za shilingi moja, tano, kumi na 20.

    Urithi wa Kenya wa wanyama wa porini unaonekana dhahiri kwenye sarafu hizo ambazo zimetolewa upya kutokana na utashi wa katiba mpya inayotaka kuondolewa kwa sura za viongozi na kuweka vivutio vya nchi.

    Wanyama walio katika sarafu hizo ni tembo, vifaru, twiga na simba ambazo zinaonekana upande mmoja kama ilivyo katika noti.

    Wakenya wamekuwa wakishinikiza sura za viongozi zilizokuwa kwenye fedha za nchi hiyo ziondolewe na badala yake ziwekwe picha za vivutio vya taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako