• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hafla ya tano ya kuwaomboleza waliouawa katika mauaji ya Nanjing yashirikisha zaidi ya watu 8,000

    (GMT+08:00) 2018-12-13 17:06:43

    Huu ni mwaka wa 81 tangu kutokea kwa mauaji ya halaiki ya Nanjing, China. Hafla ya tano ya kuwaomboleza watu waliouawa katika mauaji hayo imefanyika leo mjini Nanjing, na kuwashirikisha zaidi ya watu 8,000 kutoka ndani na nje ya China.

    Miaka 81 iliyopita, wavamizi wa Japan walikalia mji wa Nanjing uliokuwa mji mkuu wa China, na kufanya mauaji ya kikatili ya watu laki tatu, ambayo ni maumivu ya daima kwa mji wa Nanjing, na ya taifa la China. Mwezi Februari mwaka 2014, China ilitunga sheria na kuiweka tarehe 13, Disemba ya kila mwaka kuwa siku ya kuwaomboleza watu waliouawa katika mauaji hayo. Hafla ya siku hiyo ya mwaka huu imefanyika katika uwanja wa Jumba la Makumbusho ya Watu Waliouawa katika Mauaji ya Nanjing.

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, ambaye pia ni naibu spika wa baraza la kudumu la bunge la umma la China Bw. Wang Chen, alipohutubia shughuli ya kumbukumbu amesema, madhumuni ya shughuli hiyo ni kuwaomboleza watu waliouawa katika mauaji hayo, na wengine wote waliouawa na wavamizi wa Japan, na pia kuwakumbuka mashujaa wa China waliojitoa mhanga katika vita dhidi ya wavamizi wa Japan, pamoja na marafiki wa nchi nyingine waliofariki kwa ajili ya kuisaidia China katika vita hiyo. Amesema shughuli hiyo pia ni kwa ajili ya kudhihirisha msimamo thabiti wa watu wa China wa kukumbuka historia, kutosahau mambo yaliyopita, kuthamini amani na kuanzisha mustakabali mzuri, na kueleza matumaini ya China ya kushikilia kujiendeleza kwa njia ya amani. Bw. Wang anasema,

    "Katika wakati huu mtukufu, tunaweza kuwaambia watu waliouawa na mashujuaa waliojitoa mhanga katika vita hiyo kwamba, amani siku zote ni matumaini ya watu wote duniani, na amani na maendeleo ni kauli mbiu ya zama hii. Vita ni kama kioo kinachoweza kuwatambulisha watu thamani ya amani. China inapenda amani, na watu wake wanajua thamani ya amani. Itashikilia kithabiti kujiendeleza kwa njia ya amani, na daima kuwa mjenzi wa amani, mfadhili wa maendeleo, na mlinzi wa utaratibu duniani. "

    Baada ya hotuba ya Bw. Wang Chen, wajumbe 81 wa watoto na vijana wa mji wa Nanjing walisoma Azimio la Amani. Wajumbe wengine 6 waligonga Kengele ya Amani, huku njiwa 3,000 wakirusha kwa kuonyesha huzuni ya taifa la China kwa watu waliouawa na matumaini kwa amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako