• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Waziri wa kilimo aomba kuharakishwa ujenzi wa kiwanda cha mbolea

    (GMT+08:00) 2018-12-13 19:20:40

    Waziri wa kilimo nchini Tanzania bwana Japhet Hasunga ametaka shirikisho la vyama vya ushirika TFC kushirikiana na Chama kikuu cha Ushirika Njombe (Njoceru) kuhakikisha mradi wa ujenzi wa kiwanda cha mbolea unaanza mapema kabla ya Juni mwaka ujao.

    Amesema kiwanda hicho kitakapokamilika kitawasaidia wanachama na wakulima wote nchini humo kupata mbolea kwa bei nafuu.

    Hasunga aliwashauri kuandaa andiko la mradi litakaloelezea aina ya mbolea itakayozalishwa na taarifa zote zinazohitajika katika kuhanikisha mradi huo kuanza.

    Waziri huyo amesema hayo kwenye mkutano na wakuu wa bodi ya chama cha Njombe na wawekezaji kutoka China.

    Wawekezaji hao kutoka China wanataka kushirikiana na Njoceru katika ujenzi wa kiwanda hicho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako