• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kushiriki michuano ya kwanza ya Ufukweni ya Afrika nchini Cape Verde

  (GMT+08:00) 2018-12-14 09:31:31

  Kenya inatarajiwa kushiriki kwenye makala ya kwanza ya michuano ya Ufukweni ya Afrika itakayotimua vumbi Juni mwakani huko Cape Verde.

  Michuano hii ni mipya ambayo inaandaliwa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa kupitia kamati za Olimpiki za taifa. Hii ni michuno itakayotoa fursa zaidi kwa mashirikisho ya michezo kupanua majukumu yao kwa kuongeza michezo mipya itakayowapatia nafasi wanariadha ya kupata uzoefu na ushindani mpya. Mashindano haya yatashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo soka ya ufukweni, mpira wa wavu wa ufukweni, mpira wa kikapu wa wachezaji watatu kwa watatu, kuteleza baharini, tenisi ya ufukweni, handball ya ufukweni, kupiga makasia, na kuogelea. Waandaaji wanatarajia wanariadha 1,000 kutoka nchi zote 54 za Afrika kushiriki mashindano ya siku 9 ambayo yatajumuisha michezo 11.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako