• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Morocco kutoomba tena kuandaa fainali za soka za Mataifa ya Afrika mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2018-12-14 09:32:43

    Waziri wa Michezo wa Morocco, Rachid Talbi Alami amesema madhali Misri imeonyesha nia ya kuandaa fainali za soka za Mataifa ya Afrika za mwaka 2019 baada ya Cameroon kupokonywa uenyeji wa mashindano hayo nchi yake haitaomba kuandaa. Morocco na Afrika Kusini zimekuwa zikionekana kama nchi zinazopewa nafasi kubwa ya kuandaa fainali hizo zilizopangwa kuanza Juni 15. Awali, Cameroon ilizishinda nchi za Algeria na Ivory Coast na kupewa haki ya kuandaa michuano hiyo, lakini ikapokonywa uenyeji na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) mwezi uliopita kutokana na maandalizi kuchelewa kukamilika. Morocco, ambayo ilishindwa kwenye maombi ya pamoja kati ya Marekani, Mexico na Canada kuandaa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2026, imekuwa ikiripotiwa kila mara kuwa inaweza kuchukua nafasi ya Cameroon. Lakini Misri imeonyesha nia ya kuandaa mashindano hayo makubwa kwa timu za taifa kwa mara ya tano, saa chache baada ya kauli ya Alami. Fainali za mwaka 2019 za Mataifa ya Afrika zitakuwa za kwanza kushirikisha nchi 24 tangu CAF ilipopanua mashindano hayo kutoka timu 16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako