• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya na China zasaini makubaliano kuhimiza ushirikiano katika sayansi na uvumbuzi

  (GMT+08:00) 2018-12-14 10:07:37

  Wizara ya elimu ya Kenya na washauri bingwa wa China wamesaini makubaliano ili kuhimiza ushirikiano katika nyanja za sayansi, utafiti na uvumbuzi. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Kenya na Chuo cha Sayansi cha China wataunga mkono shughuli za sayansi anuai, teknolojia, uvumbuzi na ushirikiano wa elimu ya juu kati ya China na Afrika katika nyanja za ikolojia, ulinzi wa mazingira, uhifadhi wa viumbe anuai na maendeleo endelevu, pamoja na uendelezaji kupitia Kituo cha Pamoja cha Utafiti SAJOREC.

  Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Kenya Bibi Amina Mohamed amesema nchi hizo mbili zitaanzisha utaratibu mwafaka ili kuhakikisha utekelezaji wa makubaliano hayo, pia amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Kenya na taasisi za China ni kipaumbele kwa maendeleo ya Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako