• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika Mashariki zafikia makubaliano kuhimiza mafungamano

    (GMT+08:00) 2018-12-14 10:38:18

    Nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki zimefikia makubaliano ya kuhimiza mafungamano ya kikanda na biashara barani Afrika, ili kufanya biashara kati yao na nchi nyingine kuwa na gharama za chini, haraka na rahisi.

    Wawakilishi wa Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda pia wamekubaliana kwenye taarifa ya pamoja iliyotolewa mjini Nairobi, kutekeleza mageuzi ya kufanikisha biashara, ikiwa ni pamoja na kupungua "vizuizi visivyo vya ushuru" kama taratibu ngumu kuhusu bidhaa.

    Waziri wa ushirika wa Uganda Bw. Frederick Gume amesema mkutano kati ya wawakilishi wa nchi hizo ni fursa nzuri ya kuhimiza biashara ya kikanda kwa nchi nyingi za kanda hiyo ambazo hazijapakana na bahari. Shirika la biashara na maendeleo la Umoja wa mataifa UNCTAD, limesema licha ya kuwa biashara ndani ya jumuiya ya Afrika bado ni ndogo ikiwa inachukua asilimia 19.35, ni kubwa ikilinganishwa na jumuiya nyingine za kikanda barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako