• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kutimiza lengo la ukuaji wa uchumi kwa asilimia 6.5 kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2018-12-14 16:36:07

  Msemaji wa idara kuu ya takwimu ya China Bw. Mao Shengyong leo hapa Beijing amesema, mwezi uliopita uchumi wa China ulidumisha mwelekeo mzuri, na lengo la mwaka huu la ukuaji wa uchumi kwa asilimia 6.5 litatimizwa.

  Takwimu zilizotolewa na idara kuu ya takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwezi uliopita, sekta ya huduma iliendelea kwa utulivu, huku uwekezaji ukiongezeka kwa mwezi wa tatu mfululizo. Wakati huo huo hali ya ajira ilikuwa nzuri kuliko ilivyokadiriwa, na kiwango cha madeni na gharama za uzalishaji za kampuni pia kilishuka. Msemaji wa idara hiyo Bw. Mao Shengyong amesema, wakati kasi ya ongezeko la uchumi wa dunia inapungua, China imedumisha utulivu katika ukuaji wa uchumi, ajira na mfumuko wa bei. Anasema,

  "Kwanza, uchumi wa China umeongezeka kwa utulivu. Kwa upande wa uzalishaji, kuanzia mwezi Januari hadi Novemba, wastani wa kasi ya ongezeko la viwanda ulikuwa asilimia 6.3, huku sekta ya huduma ikiwa na ongezeka la asilimia 7.7 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Kwa upande wa mahitaji, katika kipindi hiki, uwekezaji kwenye miundombinu uliongezeka kwa asilimia 5.9, na wakati huo huo thamani ya mauzo ya rejareja iliongezeka kwa asilimia 9.1."

  Bw. Mao amesema, hivi sasa China imedumisha mwelekeo mzuri wa maendeleo ya uchumi, na hali hii imeweka msingi imara kwa ajili ya maendeleo ya uchumi ya mwakani. Anasema,

  "Mwaka huu, hadi sasa uchumi umeendelea vizuri, na lengo la ukuaji wa asilimia 6.5 linahakikishwa kutimizwa. Hali nzuri ya uchumi kwa mwaka huu imeweka msingi imara kwa ajili ya maendeleo ya uchumi mwakani."

  Mwezi Novemba, thamani ya ongezeko la viwanda vikubwa ilishuka kwa asilimia 0.5 ikilinganishwa na mwezi Oktoba, na hali hii imefuatiliwa na watu. Bw. Mao amechambua akisema, hali hii inatokana na kushuka kwa kasi ya ongezeko la sekta za magari, kemikali za mafuta na ekektoniki, na mabadiliko ya bei ya mafuta. Amekadiria kuwa kutokana na utekelezaji zaidi wa sera za kutuliza ajira, fedha, biashara na uwekezaji wa nje, mwakani sekta ya viwanda itadumisha maendeleo tulivu. Anasema,

  "Kuna sababu nyingi za ndani zinazoweza kuhakikisha maendeleo tulivu ya viwanda. Kwa mfano, uchumi utaendelea kwa utulivu, na sera za kuhimiza maendeleo yenye ubora zaidi ya uzalishaji na kupunguza kodi zitaendelea kutekelezwa."

  Bw. Mao pia amekadiria kuwa, mwakani matumizi ya ndani na mauzo ya bidhaa katika nchi za nje yataendelea kuongezeka kwa kasi, na uwekezaji pia utadumisha maendeleo tulivu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako