• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Balozi wa China nchini Kenya atoa makala ya kupongeza maadhimisho ya miaka 55 tangu China na Kenya kuanzisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2018-12-14 19:31:06

    Leo tarehe 14 Desemba ni siku ya kuadhimisha miaka 55 tangu China na Kenya kuanzisha uhusiano wa kibalozi. Balozi wa China nchini Kenya Bi. Sun Baohong leo ametoa makala kwenye gazeti la Daily Nation la Kenya yenye kichwa cha "kushirikiana kujenga mustakabali mpya wa ushirikiano kati ya China na Kenya".

    Bi. Sun Baohong amesema, katika miaka 55 iliyopita, uhusiano kati ya nchi hizo mbili umeendelezwa kwa kina, mawasiliano ya ngazi ya juu yamekuwa karibu, hali ya kuamiana kisiasa imeongezeka, ushirikiano katika pande mbalimbali umepanuka na kuzidisha, uhusiano huo umekuwa mfano wa kuigwa wa ushirikiano kati ya China na Afrika na ushirikiano wa Kusini na Kusini.

    Amesema, malengo ya maendeleo ya nchi hizo mbili yanalingana, na kuunganishwa kwa kupitia ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja. Hayo yametoa fursa nzuri kwa maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili. China inapenda kushirikiana na Kenya, kuhimiza uhusiano na ushirikiano wa kiwenzi na kimkakati kati yao, na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako