• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa China nchini Kenya waandaa tafrija ili kuadhimisha miaka 55 ya uhusiano wa kidiplomasia

    (GMT+08:00) 2018-12-15 17:06:27

    Ubalozi wa China nchini Kenya jana uliandaa tafrija ya kuadhimisha miaka 55 tangu nchi hizo mbili zianzishe uhusiano wa kidiplomasia, ambapo zaidi ya watu 500 wakiwemo kaimu balozi wa China nchini Kenya Bw. Li Xuhang na katibu mkuu wa muungano tawala wa Jubilee nchini Kenya Bw. Raphael Tuju.

    Bw. Li Xuhang amesema uhusiano kati ya China na Kenya unapata maendeleo siku hadi siku, na China inapenda kuimarisha ushirikiano na Kenya kwenye sekta mbalimbali.

    Bw. Tuju amesifu uhusiano uliopo kati ya Kenya na China, na kusema Kenya inapenda kuiga uzoefu wa maendeleo ya China, ili kuwanufaisha wakenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako