• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Liverpool yaigaragaza Manchester United kwa magoli 3-1 na kurudi kileleni

  (GMT+08:00) 2018-12-17 08:51:59

  Liverpool imeigaragaza Manchester United kwa magoli 3-1 na kurudi kileleni mwa Ligi Kuu England. Liverpool ilihitaji kushinda baada ya Manchester City kuichapa Everton juzi Jumamosi, na ilikuwa ni siku njema kwa Xherdan Shaqiri aliyeingia akitokea benchi katika kipindi cha pili na kumhakikishia Jurgen Klopp pointi tatu muhimu. Sadio Mane alitangulia kufunga bao dakika ya 24, akiunganisha pasi ya Fabinho, lakini ushindi huo ulidumu kwa muda mfupi baada ya makossa ya kipa Alisson kuipa Man United bao la kusawazisha wakati krosi ya Romelu Lukaku ilipompita na kumkuta Jesse Lingard aliyefunga bao la kusawazisha. Shaqiri alifunga bao lake la kwanza kwa shuti lililomgonga Ashley Young na kumpotea kipa David de Gea, na kupachika bao la pili kwa shuti lake tena kumgonga beki Eric Bailly na kumpita de Gea na kuwahakikishia wenyeji Liverpool ushindi mnono wa mabao 3-1.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako